Friday, May 25, 2012

" Mwenyekiti, Waislamu Tumezidi Kulalamika!"


Ina lilah waina ilaihi rajoon. AN-NUUR (Mwangaza)!!!!!!!!!, kweli KUN FAY KUN. Hivi muhariri wa gazeti hili ana elimu gani?. Mbona tupo waislamu wengi tu tulifanya vizuri na mpaka leo hii tuna elimu za juu kabisa.

Waislam tumezidi kulalamika sana, Wallah adui mkubwa wa waislam ni sisi wenyewe waislam. Binafsi nilipomaliza degree yangu ya kwanza na kuomba kufundisha katika shule fulani ya kiislam, nilipewa offer ya mshahara wa alfu hamsini kwa mwezi na kuambiwa kuwa nifanye for 'sabbillah'-kwa ajili ya mwenyezimungu, ukweli nilifundisha mwezi mmoja siku ya mshahara sheikh akaniita ni kupatia alfu 20, na kusema nivute subira ntalipwa zilizobakia baadae. Kilichonifanya niache kazi na kwenda klufundisha shule ya mission kwa mshahara wa laki tano ni pale nilipoona mkuu wa chuo na walezi wakigawana kila ada inapolipwa na kufanya shule kama kijiwe cha kusubiri ada na kugawana kila siku.

Kinachoua shule za kiislam ni mismanagement. Shule hizi zinaendeshwa kimfumo wa madrass za kizamani zaidi ya shule za kisasa. Na mbaya zaidi unakuta mkuu wa shule ana elimu ya dini tu elimu dunia zero unatarajia nini hapo?

Hivi kama hufundishi wanafunzi, huna walimu bora unatarajia Jibrir awashukie wanafunzi wakati wa mtihani na kuwaambia 'Ikraa bismirabika raadhi halak'? na wao kujibu maswali yote ipasavyo?, lah! hiyo ilikuwa kwa mkumbe wa mwenyezi mungu tu Mtume Muhhamad (SAW). Bila maandalizi bora kwa wanafunzi hawawezi kufaulu.

Tuache kushabikia ujinga maana hata ukimpatia mtoto asiyejua kusoma dision one kwa ajili ya kuwafurahisha akina Sheikh Majaka wa An-nuur bado huko juu hatafika popote.

Heading kama hizi za An-nuur ndizo zinazidi kudidimiza elimu miongoni mwa waislam. Watoto wanaacha kusoma kwa bidii wakidhania kuwa majina yao ndiyo yatawafanya wafeli wakati mitihani inaandikwa namba mpaka stage ya mwisho kabisa baada ya kusahihishwa ndiyo majina yanawekwa kwa ajili ya kudisplay matokeo. Mimi nilifaulu la saba, nikaenda shule ya sekondari maalum ya serikali, nikafaulu form four kwa daraja la kwanza, nikafaulu form six kwa taraja la kwanza, nikafaulu, chuo kwa taraja la pili la juu, nikafaulu masters kwa daraja la kipekee (distinction), nimemaliza PhD kwa minor corrections, na majina yangu yote matatu ni 100% ya kiislamu.

Hii stori ya An0nuur imenikwaza sana Wallah, waandishi kama hawa ndiyo wanaudhalilisha uislam bila kijiju.

Mjumbe.

No comments:

Post a Comment