Written by Ado Shaibu at udsm |
1.kwamba katika uandikaji wa katiba zote,wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.kwa mfano,katika uandikaji wa katiba ya mwaka 1977,wananchi hawakushirikishwa ipasavyo kutoa maoni yao.Hata wana CCM hawakushiriki kwa sababu chombo kikuu cha chama hicho,yaani mkutano mkuu,hakikuhusika.Iliyohusika ni halimashauri kuu.Jadi ya CCM ni kuyafanya yale yanayozungumzwa humo kuwa siri.
2.kwamba kutokana na kutoshirikisha wanachi ipasavyo,katiba zote zimekosa uhalali wa kisiasa(political legitmacy).lakini prof.shivji anataadharisha kwamba hii haimaanishi kwamba utawala wa mwalimu nyerere ulikosa uhalali wa kisiasa.uhalali ulikuwepo,bali haukutokana na katiba.ulitokana na itikadi ya CCM pamoja na umahiri na umaarufu wa mwalimu mwenyewe!
3.kwamba hata uhalali wa kisheria(legal legitimacy) una walakini!.kwa mujibu wa pro.shivji,historia ya utungaji wa katiba imejaa upuuzwaji na upindishaji wa hapa na pale wa matakwa ya kisheria.
4.kwamba hakukuwa na mjadala wa kitai katika utungaji wa katiba zote.Angalau,mjadala wa kitaifa ulikuwepo katika mabadiliko ya katiba ya mwaka1984 ambapo haki za binadamu ziliingizwa kwenye katiba.
Fikra hizi za prof.shivji pia zimefanyiwa tafakuri ya kina katika kitabu chake kipya kiitwacho INSHA ZA MAPAMBANO YA WANYONGE (hasa kwenye mada iitwayo "Madai ya katiba mpya:Unyonge wa katiba au Katiba ya wanyonge?''